Utangulizi:

Wizara ya Fedha na Mipango inatekeleza majukumu kwa kuzingatia katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 pamoja na marekebisho yake. Sheria mbalimbali inazozisimamia na miongozo ya Serikali.

Taasisi ziliopo chini ya Wizara ya Fedha na Mipango kwa upande wa Pemba ni:-

 1. Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ)
 2. Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB)
 3. Mamlaka ya Mapato (TRA)
 4. Mamlaka ya Ununuzi na Uondoaji wa Mali za Serikali (ZPPDA)
 5. Mamlaka ya Vitega Uchumi (ZIPA)
 6. Mfuko wa Hifadhi wa Jamii (ZSSF)
 7. Tume ya Mipango
 8. Ofisi ya Takwimu Mkuu wa Serikali
 9. Shirika la Bima

Programu: Uendeshaji na uratibu wa Wizara ya Fedha na Mipango

Matokeo ya muda mrefu: Kuimarisha kwa utendaji katika Wizara ya Fedha na Mipango.

Programu Ndogo: Uratibu wa utekelezaji wa shughuli za Wizara Pemba.

Lengo Kuu: Kuhakikisha shughuli zilizopangwa kwa Sekta ya Fedha Pemba zinatekelezwa.

Huduma:

 1. Kusimamia na kuratibu shughuli za uendeshaji wa Wizara kwa upande wa Pemba.
 2. Kusimamia shughuli za utunzaji wa mali za Serikali na mitaji ya Umma.
 3. Kusimamia na kutoa huduma za Uhasibu kwa upande wa Pemba.
 4. Kuratibu masuala ya bajeti, sera za fedha na kodi na masuala ya fedha za nje kwa upande wa Pemba.
 5. Kusimamia masuala ya ukaguzi wa ndani wa Hesabu za Serikali.

Ofisi kuu Pemba imeundwa na Idara Kuu 5.

 1. Idara ya Utumishi na Uendeshaji
 2. Idara ya Mitaji ya Umma
 3. Idara ya Mipango, sera za fedha na kodi pamojana Fedha za nje
 4. Idara ya Hazina ndogo
 5. Idara ya Ukaguzi wa ndani

 

In case you need help

*
 

Question? Call

Our support is available on Weekdays
Monday-Friday: 8am to 3pm
Saturday-Sunday: Weekend

 

Need support?

For more support u can visit our website www.mofzanzibar.go.tz or write us an email info@mofzanzibar.go.tz

 

Testimornial

Bellow are some interesting links for you! (under costruction)
Learn more...